

Kurejeshwa kikosi cha kwanza beki Juma Abdul, kumeongeza ufanisi upande wa kulia timu inaposhambulia
Mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania, Abdul alihusika kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Mrisho Ngasa
Krosi zake zilisababisha madhara langoni kwa Polisi Tanzania
Pengine hii ndio sababu iliyofanya mashabiki kuhoji kukosekana kwake kwenye kikosi kwani mchezo wake wa kwanza tu, amedhihirisha bado ni mtu muhimu sana Yanga
Bila shaka mechi ya leo dhidi ya Coastal Union, ataendeleza pale alipoishia juzi
Yanga inahitaji ushindi leo. Krosi zake pamoja na uwepo wa mshambuliaji David Molinga ambaye ni hatari kwa mipira ya vichwa, ni habari mbaya kwa Coastal Union




0 Comments