

Simba bado haijakata tamaa kumuwania mshambuliaji wa Nkana Fc Walter Bwalya licha ya timu yake kutaka mkwanja mrefu
Inaelezwa uongozi wa Simba tayari umefikia makubaliano binafsi na Bwalya, lakini kikwazo kimebaki kwa Nkana ambayo inataka ilipwe si chini ya dola laki nne (zaidi ya Milioni 800) ili iweze kumuachia
Bwalya bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Nkana Fc
Aidha Nkana Fc iko tayari 'kuvunja-vunja' kwa kupokea fedha na mchezaji, hata hivyo mmoja wa viongozi wa Simba amesema bado fedha wanazotaka walipwe ni nyingi
Simba inakimbizana na muda kukamilisha usajili wake kwani mpaka Juni 30 inapaswa kuwa imewasilisha majina kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao



0 Comments