MSHAMBULIAJI wa Mtanzania, Uhuru Selemani amejiunga na timu ya Lupopo FC ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu ya DR Congo.
Nyota huyo wa zamani wa Simba awali alikuwa akikipiga katika kikosi cha Royal Eagles cha Afrika Kusini kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo ambapo alikitumikia kwa miaka minne.
Hivyo, anaungana na Watanzania wengine ambao ni Eliud Ambokile, Ramadhan Singano ambao wapo TP Mazembe na timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya DR Congo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Uhuru alisema kuwa ameondoka Sauz na kwenda Congo sababu ya kuwa mbali na familia pamoja ubaguzi ambao alikuwa anapata nchini humo.
“Ni kweli nimeondoka Royal Eagles nawashukuru kwa ushirikiano wao mpaka nimefika hapa kwa sasa nipo Lupopo FC kwa mkataba wa miaka miwili, nitakuwa hapo kupambana.
“Nitakuwa karibu na familia yangu, pia kuondokana na suala la ubaguzi pamoja na machafuko ya Xenophobia, lakini namshukuru Kocha Selemani Matola (wa Polisi Tanzania) amekuwa akinipa moyo wa kutokata tamaa,” alisema Uhuru.
Stori na Martha Mboma, Championi
The post Xenophobia yamkimbiza Uhuru Sauz, atua Congo appeared first on Global Publishers.
0 Comments