KIKOSI cha Taifa Stars, jana Alhamisi kilirejea jijini Dar es Salaam kikitokea Bujumbura nchini Burundi kilipoenda kucheza dhidi ya Burundi katika mchezo wa Hatua ya Awali ya Kufuzu Kombe la Dunia 2022.
Katika mchezo wao, Taifa Stars ilitoka sare ya bao 1-1 na Burundi ambapo timu hizo zinatarajiwa kurudiana keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Msafara wa Taifa Stars ulipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, uliwashangaza wengi kwani ulifuatana na wa kikosi cha Burundi kutokana na timu hizo kupanda ndege moja kuja Tanzania kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi.
Mara baada ya kuwasili, Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, alitoka moja kwa moja kuelekea kwenye gari lililoandaliwa kuwachukua na kushindwa kuzungumza chochote.
Wakati Ndayiragije akiondoka bila ya kuzungumza jambo, Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, alisema: “Kikubwa tunashukuru mchezo wa kwanza tumeumaliza salama kwa matokeo ambayo si mabaya sana. Tunajipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa hapa nyumbani ili kusonga mbele.
“Hatupo tayari kuona tunapoteza nyumbani, kila mmoja wetu hapa anatamani kuona tunashinda na kusonga mbele. Tunaona Watanzania waendelee kutusapoti ili tufikie malengo.”
Kuhusu kutoingia vyumbani katika mchezo wa juzi, Samatta alisema: “Tulipewa taarifa kuwa hakukuwa salama kwetu kutumia vyumba hivyo, lakini kwa mazingira ya soka la Afrika vitu kama hivyo huwa vinatokea, tunaachia mamlaka husika kushughulikia hilo suala.”
Mshindi wa jumla katika mechi hizi mbili, atatinga hatua ya makundi
The post VIDEO: Taifa Stars, Burundi Watua Dar Pamoja, SAMATTA, MSUVA Wazungumza! appeared first on Global Publishers.
0 Comments