Kikosi cha Simba kimevunja mwiko Kaitaba Stadium kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar, baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Kagera Sugar kwa misimu miwili mfurulizo.
Ushindi huo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) umepatikana baada ya Simba kukubali kichapo mara mbili mfululizo kutoka kwa walima miwa hao msimu uliopita.
Bao la kwanza la Simba limewekwa kambani na Meddie Kagere kwa mpira wa kichwa mnamo dakika ya tano, akipokea pasi maridhawa kutoka kwa Deo Kanda. Dakika ya 35, Mohammed Hussein naye aliingia kambani kwa kumalizia pasi nzuri ya Kagere na kuweza kuielekeza kambani moja kwa moja.
Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, Simba ilikuwa mbele kwa mabao hayo 2-0, Kipindi cha pili kilianza kwa Kagera kuamka wakisaka bao kwanza lakini jitihada zao ligonga mwamba kutokana na uimara wa Simba eneo la ulinzi.
Katika dakika ya 78 tena, Kagere aliingia kambani kwa njia ya penati baada ya Miraji Atumani kufanyiwa madhambi eneo la hatari.
Matokeo yaifanya Simba izidi kuwa kileleni kwa kufikisha jumla ya alama tisa (9) sawa na Kagera lakini Simba wakiwa juu kwa faida ya kuwa na mabao mengi huku Kagere akifikisha mabao 5 kwa mechi 3 alizocheza.
The post Simba Yavunja Mwiko, Yaichapa Kagera 3 Kavu appeared first on Global Publishers.
0 Comments