KENEDDY Juma, beki kisiki wa Simba maarufu kama mwili jumba amesema kuwa bado Simba ina nafasi ya kutetea kombe lao kutokana na kasi waliyonayo.
Simba leo imefanikiwa kutwaa pointi tatu mbele ya Biashara United kwa ushindi wa mabao 2-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Karume.
“Tuna muunganiko mzuri na kikosi kinazidi kuimarika hivyo nafasi ni kubwa kwetu kutwaa ubingwa msimu huu, sapoti ya mashabiki ni muhimu,” amesema.
Huu unakuwa ni mchezo wa nne kwa Simba kushinda na ukiwa ni wa pili kwa mlinda mlango, Aishi Manula kutoka na clean Sheet baada ya kwanza kuipata mbele ya Kagera Sugar.
Msimu uliopita uwanja wa Karume, Simba ilishinda mabao 2-0 mbele ya Biashara United na yalifungwa na John Bocco huku leo wafungaji wakiwa ni Meddie Kagere na Miraj Athuman.
The post Simba Yaipiga Biashara United Bao 2-0 Nyumbani appeared first on Global Publishers.
0 Comments