MANCHESTER United inaaminika inamwania kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino. Mkataba wa Pochettino kwa klabu yake ya Spurs inasemekana unatoa mwanya kwa klabu inayomhitaji kutoa kiasi cha pauni milioni 32.
Pochettino kwa sasa yupo katika presha kubwa kwenye klabu ya Tottenham kutokana na mwenendo wa kusuasua wa timu hiyo. Wasiwasi wa mustakabali wake umeongezeka zaidi kufuatia kitendo cha timu hiyo kutolewa na Colchester kwenye michuano ya Kombe la Carabao.
Pamoja na kutolewa huko, pia timu hiyo majuzi ilifungana mabao 2-2 na Olympiakos ya Ugiriki kwenye Ligi ya
Mabingwa Ulaya lakini kiwango chao kwenye ligi kimekuwa cha chini.
Manchester United, ambayo inadaiwa imechoshwa na kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer inasemekana inajipanga kujitosa kwa Pochettino.
Klabu hiyo inadaiwa imeanza kuwasiliana na Spurs ili kulipa pesa na kumchukua Pochettino na kuachana na Solskjaer. Pochettino mwenyewe amekiri yupo katika kipindi kigumu katika klabu ya Tottenham.
The post Man United Yampigia Hesabu Kocha wa Tottenham appeared first on Global Publishers.
0 Comments