Windows

Liverpool, Chelsea Waanza na Kipigo Ligi Ya Mabingwa Ulaya

LIGI ya Mabingwa Ulaya kwa hatua ya makundi ya 2019/2020 imeanza jana Septemba 17, 2019 kwa kushuhudia rekodi mbalimbali zikiwekwa. Bingwa mtetezi Liverpool amefungwa katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Napoli Liverpool ikilala kwa bao 2-0 ugenini.

Chelsea wakiwa nyumbani wamekosa Penati na kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Valencia.

Jumla ya magoli 21 yalifungwa katika mechi 8 zilizochezwa usiku wa jana ikiwa ni idadi kubwa kabisa katika mechi za ufunguzi.

Mbwana Ally Samata nahodha wa Taifa Stars ameingia katika rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika michuano hiyo mikubwa kabisa na yenye fedha nyingi duniani katika soka.

Pia Samata amekuwa Mtanzania Wa kwanza kufunga bao katika michuano hiyo akifunga moja kati ya mabao mawili waliyopata Genk katika kipigo cha bao 6-2.

 

Akiwa pia mmoja kati ya wachezaji Wa kwanza kufunga katika mechi zao za kwanza katika michuano hiyo.

 

Genk imekuwa moja kati ya timu zilizofingwa mabao mengi zaidi kipindi cha kwanza mana mpaka mapumziko walishafungwa bao 5-1 na mechi ikaisha kwa kufungwa bao 6-2.

Erling Braut Haaland amefunga hat-trick katika mechi yake ya kwanza katika mashindano hayo tena ndani ya Dakika 45 akiichezea Salzburg katika ushindi Wa bao 6-2 walioupata dhidi ya Genk.

 

Lionel Messi amerejea baada ya kuwa majeruhi na kukaa nje ya uwanja kwa siku 115, Barcelona wakinusurika kichapo nyumbani kwa Dortmund kipa Wa Barca Marc-André ter Stegen akipangua Penati ya Marco Reus

 

Ansu Fati amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kabisa wa Barcelona kucheza katika michuano hiyo akianza katika mechi ya Jana dhidi ya Borrussia Dortmund akiwa na umri Wa miaka 16 na siku 351.

 

The post Liverpool, Chelsea Waanza na Kipigo Ligi Ya Mabingwa Ulaya appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments