Windows

Licha ya Kipigo… CAF Yaitengea Yanga Mil.774

TIMU ya Yanga kama ingefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika juzi Jumamosi ingejinyakulia dola 550,000 (zaidi ya Sh 1.5 bilion), lakini kwa kuwa inaendelea na michuano ya kimataifa, huenda ikakomba kitita cha dola 275,000 (zaidi ya Sh milioni 774) kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

 

Zesco United iliitupa Yanga nje ya michuano hiyo kwa jumla ya maba 3-2. Hata hivyo, bado Yanga ina nafasi nyingine ya kujinyakulia mamilioni kutoka Caf. Mamilioni hayo ni yale ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo sasa itashiriki baada ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Endapo itafanikiwa kitinga hatua ya makundi katika michuano hiyo itajinyakulia dola 275,000 (zaidi ya Sh 774 milioni).

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Yanga kupitia kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela umeliambia Championi Jumatatu kuwa sasa wanajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo.

 

“Lengo letu lilikuwa ni kufika hatua ya makundi katika michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini imeshindikana, sasa nguvu zetu tunazihamishia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kama uongozi tutahakikisha tunafanya kila liwezekanalo ili tuweze kutinga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo,” alisema Mwakalebela.

The post Licha ya Kipigo… CAF Yaitengea Yanga Mil.774 appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments