Windows

Aussems: Siachi Pointi Kokote

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji, ametamba safari hii haachi pointi kwa timu yoyote ile atakayocheza nayo bila ya kujali ni ugenini au nyumbani.

 

Aussems ambaye ameiongoza Simba kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi tisa, ametamba kwamba atakusanya pointi kwenye michezo yao 35 ambayo imebakia ya Ligi Kuu Bara.

Michezo hiyo ni kabla ya jana Jumapili Simba haijacheza dhidi ya Biashara United kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara.

 

Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa kwa safari hii hataki kuacha alama yoyote kwa wapinzani wake ambapo amepanga kushusha vipigo kwa timu yoyote atakayokutana nayo.

“Tulipata pointi tatu kwenye mechi zetu tatu za mwanzo, lakini tunategemea kupata pointi tatu nyingine kwa wapinzani wetu ambao tutakutana nao katika michezo ya mbele.

 

“Tulichopanga ni kutopoteza pointi katika mechi yoyote na nimekuwa nikiwakumbusha wachezaji juu ya hilo ndiyo maana wanapambana katika mechi zetu. Lengo ni kutwaa ubingwa kwa sababu hiyo ndiyo furaha yetu pekee ambayo tunayo hasa baada ya kutoka kimataifa,” alisema Aussems. 

The post Aussems: Siachi Pointi Kokote appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments