TAJIRI wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amewathibitishia mashabiki wa klabu hiyo kwamba mwezi ujao viwanja vya nyasi bandia na asilia vitakuwa tayari.
Mo alifanya ziara kwenye Uwanja huo uliopo Bunju, Dar es Salaam jana Jumamosi asubuhi kushuhudia maendeleo ya ujenzi ambapo aliridhishwa na kusisitiza kwamba sasa mambo yameiva.
Tayari nyasi bandia pamoja na gundi za kubandikia nyasi hizo zimeshafika na kazi rasmi itaanza leo Jumatatu, kisha badae Oktoba timu itahamia huko.
MO aliahidi kufikia msimu huu timu hiyo ingekuwa imeshaanza kutumia viwanja vyake vya Bunju kwa ajili ya mazoezi huku akiahidi maendeleo zaidi kwenye miundombinu mbalimbali ya Simba.
“Nina habari njema,kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba,Uwanja wa nyasi asilia na nyasi bandia pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo vitakuwa vimekamilika, inshallah,”alisema Mo.
Aliongeza kuwa; “Natarajia kuona timu ikifanya mazoezi hivikaribuni.” Kama Simba ikifanikisha hilo itakuwa imepiga hatua kubwa na kuwapiga bao Yanga ambao ni watani zao wa jadi. Yanga waliahidi kuwa
The post Mo: Tunahamia Kwenye Pichi Yetu Oktoba appeared first on Global Publishers.
0 Comments