

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mafanikio ya kuungwa mkono klabu ya Simba yanayopatikana sasa hayakuja kwa bahati mbaya
Baada ya Yanga kushindwa kujaza hata robo ya uwanja wa Taifa kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wamemshushia lawama Afisa Habari wao Dismas Ten kuwa hawajibiki ipasavyo
Manara amewapa somo mashabiki wa timu hiyo kuwa suala la kujaza uwanja wa Taifa halitokei tu, bali linahitaji mipango
"Tulikuwa na mipango thabiti ya kukuza na kuitangaza 'brand' yetu ya Simba kwa mashabiki," amesema Manara
"Wapo waliotubeza wakati tunaanza, lakini sasa kila mmoja anatamani kuwa kama sisi"
"Simba ndio klabu yenye ufuasi mkubwa kupita zote Afrika Mashariki na ya kati. Na ndio klabu pekee inayojaza Washabiki elfu sitini katika mechi zake kubwa zote kwenye ukanda huu"
"Tumeongeza ufuasi huu baada ya kuwa na mipango madhubuti na endelevu iliyoratibiwa kistadi mno na uongozi wa klabu"
"Na sasa tunakwenda kutengeneza mpango mahsusi wa mashabiki ili tujue wapo wapi na wanafanya nini"
"Mpango huu utatuwezesha sio tu kujua idadi yetu lakini pia utaiingiizia klabu pesa na kuzidi kuwa juu hapa nchini"
"Yatajwa kwa sasa katika kila watanzania kumi ,saba hadi nane ni wafuasi wa Simba!"



0 Comments