Windows

Ajib, Manula kurejea kikosini wiki hii



Fundi wa mpira Ibrahim Ajib na mlinda lango Aishi Manula wanatarajiwa kurejea kikosini wiki hii kuendelea na maandalizi ya mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Daktari wa Simba Yassin Gembe, Ajib na Manula wako kwenye hatua za mwisho za matibabu yao

Lakini ni wazi wataukosa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumamosi, August 17 2019

Aidha mshambuliaji Wilker Da Silva yeye hali yake bado na anaendelea na matibabu

Post a Comment

0 Comments