Polisi waliwaonya waandamanaji dhidi ya kubadili njia iliyokubaliwa kwa ajili ya maandamano ya Jumamosi, wakisema wataingilia kati ikiwa waandamanaji watashindwa kutii amri hiyo.
Lakini waandamanaji hawakutii amri na hivyo kuweka vizuizi barabarani na kuathiri usafiri wa umma. Waandamanaji hao wanasema serikali inapaswa kusimama na kusema chochote la sivyo maandamano ya kila siku yanazidi kuwa hatari na kugeuka kuwa ya machafuko.
Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi katika eneo la tsim Sha Tsui ambalo lina maduka ya kifahari.
Wakati maandamano yakiendelea hadi leo asubuhi, polisi wamelazimika kufyatua tena gesi ya kuwasha wakati waandamanaji wakijaribu kukabiliana na polisi.
0 Comments