Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems aliwatumia pamoja viungo Sharaff Shiboub na Jonas Mkude kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo uliopigwa juzi Jumamosi, August 10
Kulikuwa na changamoto katika kujipanga kwa viungo hao ambapo mara kwa mara walijikuta wako nje ya nafasi za majukumu yao
Ni changamoto hiyo ambayo iliwapa nafasi UD Songo mara kwa mara kupenyeza mipira kupitia katikati
Lakini sababu kubwa wachezaji hao walikosa maelewano kwa kuwa hawajacheza pamoja vya kutosha
Ikumbukwe Mkude aliondoka kambini Afrika Kusini kurejea nchini kujiunga na timu ya Taifa wakati Shiboub na wachezaji wengine wakiendelea kujifua nchini humo
Aussems aliwapanga viungo hao pamoja kutokana na umahiri walionao
Shiboub ameongeza ubunifu kwenye safu ya kiungo ya Simba, anaweza kucheza chini au juu
Ana uwezo mzuri wa kukaba lakini pia ni mzuri sana kwenye kupiga pasi
Msaada wake uko pande zote, timu inapokuwa na mpira na bila ya mpira
Timu ikiwa na mpira uwezo wake wa kupiga pasi unainufaisha timu lakini hata ikiwa haina mpira ni mahiri sana katika kukaba
Wakiendelea kucheza pamoja na Mkude katikati, baada ya muda wataifanya Simba iwe ngumu sehemu ya kiungo
Hii itawapunguzia majukumu akina Clatous Chama, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajib na Francis Kahata kufanya kazi ya kuwatengenezea nafasi akina Meddie Kagere, John Bocco na Deo Kanda
0 Comments