Windows

Aussems hana wasiwasi kabisa na UD Songo



Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems , amesema anaamini kikosi chake kitatumia vizuri ardhi ya nyumbani kuiondosha mashindanoni UD Songo na kutinga raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba juzi ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya UD Songo ya Msumbuji, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Jiji la Kibiashara la Beira, Msumbiji.

Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo, utachezwa Agosti 25 mwaka huu, Uwanja wa taifa, Jijini Dar es Salaam.

Ili kusonga mbele, Simba inahitaji ushindi,huku wapinzani wao wakihitaji matokeo ya sare ya mabao kwa kuzingatia kigezo cha bao la ugenini.

Aussems alimesema walikusudia kupata ushindi ugenini, lakini wakakwama na sasa wanajipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani.

Alisema, amewasoma vizuri wapinzani wao na kubaini kasoro kadhaa ambazo ana amini watazitumia kupata ushindi katika mchezo wa marudiano.

"Sina muda wa kupoteza tena ndio maana tumerudi na kuanza mazoezi haraka, hii michuano ni migumu," Aussems aliliambia Mtanzania

"Ili kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele tulipaswa kushinda ugenini na nyumbani. Jambo la kujivunia ni kwamba nyumbani tutacheza tukiwa na mashabiki wetu ambao wana maana kubwa katika kufanikisha ushindi wetu"

"Pia unaweza kuona mazingira ya uwanja tuliochezea mechi ugenini ni tofauti na Taifa ambao unaruhusu kuucheza mchezo wetu"

Aussems amesema tofauti na msimu uliopita ambapo malengo yalikuwa kufika hatua ya makundi lakini wanafanikiwa kufika robo fainali, safari hii wamejiandaa kwa mapambano ya kuwania ubingwa.

Post a Comment

0 Comments