BAADA ya kupoteza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Mtibwa Sugar, imeanza kuipigia hesabu Simba watakayokutana nayo Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mechi iliyopita, Mtibwa walichezea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Lipuli FC katika mchezo uliopigwa Agosti 24, mwaka huu, Uwanja wa Samora, Iringa.
Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, alisema wana muda mrefu wa kufanya maandalizi ya mchezo huo, lengo likiwa ni kutorudia makosa waliyofanya kwa Lipuli.
“Mchezo wa pili wa ligi tunakutana na Simba, tutakuwa ugenini, lakini tunajiandaa kukabiliana nao, matokeo yaliyopita sisi hayatuhusu, tunachohitaji ni pointi,” alisema.
Alisema kuanza vibaya kumewapa hasira, atafanya marekebisho makosa yaliyojitokeza mechi ya nyuma, kuhakikisha hayajirudii kwa Simba.
0 Comments