Windows

Kocha Mwadui FC ashtuka


BAADA ya kusikia kuwa timu zitakazoshuka daraja msimu huu ni nne, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Khalid Adam, amesema kuanzia sasa kila mechi kwake itakuwa ni fainali.

Hivi karibuni, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi, walisema kuwa msimu huu zitashuka timu nne za Ligi Kuu Bara na mbili kucheza ‘play off’ ili msimu ujao zibaki 16 kati ya 20 zinazoshiriki sasa.

Adam aliliambia BINGWA jana kuwa hakuna muda wa kulala, kwani ligi hiyo itakuwa ngumu zaidi ya misimu kadhaa iliyopita, kila mmoja akikwepa kushuka daraja.

Alisema licha ya kuanza ligi hiyo kwa ushindi, wakiifunga Singida United bao 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, hawatabweteka.

Kocha huyo alisema mchezo wa kwanza umemuonyeshea picha halisi ya ligi kuwa kila timu imejipanga, hivyo kupata ushindi si rahisi.

“Msimu huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutoshuka daraja, inatakiwa kuanza mapambano mapema, kitendo cha kushuka timu nne na mbili kucheza ‘play off’, si masikhara,” alisema.

Alisema mechi ijayo wanacheza na Ndanda FC ugenini, Septemba14, mwaka huu, lakini hawana muda wa kupumzika wanaendelea na mazoezi hadi siku ya kusafiri kwenda Mtwara

Post a Comment

0 Comments