

STAA, Leroy Sane amepata matumaini ya kucheza tena ndani ya msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti na maendeleo kuwa vizuri.Fowadi huyo wa Manchester City hajataka kuwa mudfa ambao atakuwa amerudi uwanjani, lakini matumaini yamekuwa makubwa baada ya upasuaji wa kutibu tatizo lililokuwa likimsumbua kufanyika kwa mafanikio.
Sane alienda kufanyiwa upasuaji huko Austria na kuachana na daktari anayependelewa zaidi na klabu ya Man City kwenye upasuaji, Dr Ramon Cugat wa huko Barcelona. Amekwenda kwa profesa Christian Fink baada ya kushauriwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ujerumani.
Austria kwa sasa ndiko mahali panapodaiwa kuwa ni salama zaidi kwa wachezaji wenye matatizo kama ya Sane, ambapo madaktari wamekuwa mahiri zaidi kwa sababu uwepo wa barafu na michezo ya kuteleza kwenye theluji yamefanya kukithiri kwa majeruhi ya aina hiyo.
Uamuzi wa Sane ulikuwa binafsi na kwamba hauhusiani na Bayern Munich ambao walidaiwa kuifukuzia sana saini yake katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi kabla ya majeruhi kutibua kila kitu. Man City wamedai kwamba Sane anauzwa Pauni 135 milioni.



0 Comments