Windows

Luiz apewe ruhusa kupiga mipasi mirefu

.KOCHA wa Arsenal, Unai Emery amesema kwamba amemruhusu beki David Luiz kucheza ile mipira yake mirefu na soka la moja kama alilokuwa akicheza huko Chelsea, wala haina shida.

Kocha Emery anataka Luiz aingize radha tofauti kwenye kikosi chake hasa kutokana na kutaka kuwatumia mabeki wake wa kati kuucheza mpira. Katika kipindi chake cha pili huko Chelsea, Luiz mara kadha ameonekana akipiga pasi ndefu kwa Pedro na kuwa beki wa kati aliyetengeneza nafasi nyingi za mashambulizi kuliko mwingine yeyote kwa msimu uliopita, nafasi 11.

Kwa mujibu wa Telegraph, kocha Emery amemwambia Luiz awe anapiga pasi hizo ndefu kwa straika Pierre-Emerick Aubameyang akiamini kwamba wawili hao watatengeneza kombinesheni bora kabisa katika kuifanya timu hiyo kuwa bora.

Wachezaji hao wawili, Luiz na Aubameyang wote walitarajia kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool huko Anfield. Kocha Emery amefichukua kufurahishwa sana na kitendo cha Luiz kwenda kujiunga na timu yake baada ya kuwa naye pamoja huko Paris Saint-Germain.

Beki huyo Mbrazili aliamua kutimka na kuachana na Chelsea baada ya kuambiwa na kocha mpya Frank Lampard kwamba atakuwa chaguo la nne kwenye beki ya kati nyuma ya Kurt Zouma, Andreas Christensen na Antonio Rudiger.

Post a Comment

0 Comments