

UONGOZI wa KMC umesema kuwa umejipanga kufanya kweli Agosti 23 Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya AS Kigali ya Rwanda.
Mchezo wa awali KMC ilikubali kupata sare ya bila kufungana, wana kazi kubwa ya kutafuta ushindi mchezo wa marudio ili kusonga hatua inayofuata.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anuary Binde amesema kuwa kwa sasa kila kitu kinakwenda sawa ni jambo la wakati tu kwa wachezaji kuonyesha maajabu.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu kwani mchezo wa kwanza tulitoka nao sare kwao kwa kuwa wanakuja nyumbani basi hakuna namna lazima tufanye kweli.
"Wachezaji wapo tayari na wana morali kubwa makosa madogo benchi la ufundi linayafanyia kazi na ni wakati wa mashabiki kutupa sapoti ya kutosha," amesema.



0 Comments