

Beki wa kulia wa Yanga Paulo Godfrey 'Boxer' wakati wowote atajiunga na kambi ya timu hiyo mkoani Kilimanjaro baada ya kupona majeraha
Boxer aliumia kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers na alibaki jijini Dar es salaam kuendelea na matibabu
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hali ya mchezaji huyo inaendelea vizuri na kesho anaweza kusafiri kuelekea Moshi
Tayari mkongwe Juma Abdul ameripoti kambini kuongeza nguvu upande wa kulia
Aidha akizungumzia maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers, Zahera amesema ari ya wachezaji wake iko juu na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri nchini Botswana
"Ari ya wachezaji iko juu, nimezungumza nao mmoja mmoja, nafikiri tutafanya vizuri Botswana"
Yanga imeweka kambi Moshi ikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa August 23, Gaborone Botswana



0 Comments