

Msimu uliopita safu ya ushambuliaji ya Simba iliyokuwa ikiundwa na Meddie Kagere, John Bocco na Emmanuel Okwi ilikuwa moto wa kuotea mbali
Washambuliaji hao walifunga mabao 53 kwenye ligi
Hata hivyo Simba imeanza kampeni msimu huu ikiwa na washambuliaji wawili Meddie Kagere na John Bocco baada ya Okwi kutimkia Misri
Katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo, Bocco na Kagere walianza pamoja huku Francis Kahata na Clatous wakiungana nao wakitokea pembeni
Hata hivyo kocha Mkuu wa mabingwa hao wa nchi Patrick Aussems amekiri bado hajapata mtu sahihi wa kuziba nafasi ya Okwi
Akizungumza jana kwenye mazoezi ya Simba yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam, Aussems alisema anawaangalia Deo Kanda na Francis Kahata ili kutengeneza muunganiko na Bocco na Kagere
Amesema kwa uwezo unaoonyesha na wachezaji hao, anaamini baada ya muda safu ya ushambuliaji ya Simba itarejesha makali yake ya msimu uliopita



0 Comments