Windows

Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko mkombozi kwa Wakulima


Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni mkombozi kwa wakulima hapa nchini.

Hasunga ameyasema hayo alipotembelea banda la bodi hiyo kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu ambako kunafanyika maonesho ya Nanenane kitaifa ambapo wakulima wanaonesha mazao yao lakini pia maonesho hayo yanatumika kuwaunganisha na wadau mbalimbali wa kilimo.

“Kwa wakulima bodi hii ni mkombozi kwa wakulima kwani jukumu lake ni kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa mazao ya nafaka, lakini pia bodi hii inanunua mazao ya nafaka na kuyaongezea thamani na sasa wameanzisha kiwanda kule Arusha cha kusaga nafaka na kuuza, lakini pia Dodoma watajenga kiwanda cha kuchakata Alizeti na nafaka na pia Mwanza watajenga kiwanda cha kuchakata mpunga na mazao mengine hivyo bodi hii ni muhimu kisekta.” Alisema.

Hasunga pia ameipongeza Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa kutekeleza vema maelekezo ya Serikali ya kununua na kuuza Korosho.

"Moja ya Jukumu tulioipatia Bodi mwaka huu ni kununua na kuuza Korosho kwa niaba ya Serikali na kazi hiyo wameifanya vizuri, wameweza kunua Korosho yote na wanayo," alifafanua.

Alisema, Bodi kama wafanyabiashara imeweza kununua Korosho na kuongeza thamani (Ku- process) kwa kuziweka kwenye vifungashio vya viwango mbalimbali na ndio maana wako kwenye
maonesho ili kuzionesha na kutangaza masoko mbalimbali kwa wadau wa ndani na nje ili waweze kutoa Oda na hii itasaidia kupanua masoko ya Korosho.

Maonesho ya Nanenane kitaifa hapa Nyakabindi Mkoani Simiyu yalizinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Agosti 1, na yatafikia Kilele Agosti 8, 2019 na yamebeba kauli mbiu isemayo “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa ukuaji w aUchumi wa Nchi.”.



Post a Comment

0 Comments