Windows

Bodi ya Utalii yaahidi 'kuibeba' Rock City Marathon


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ili kuhakikisha kuwa mbio hizo zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani hapa nchini.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TTB, Geofrey Tengeneza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi ameeleza hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.

"Kwa kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizi nitamke bayana kuwa TTB tupo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema.

Hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye viunga vya ofisi za TTB jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo.

Tengeneza pia alithibitisha ushiriki wake Pamoja na viongozi waandamizi wa bodi hiyo kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jingo la kibishara la Rock City Mall, jijini Mwanza ambapo washiriki wa mbio hizo watapita katika barabara mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika viunga hivyo.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)..

Post a Comment

0 Comments