

Uongozi wa klabu ya Yanga umetuma maombi Bodi ya Ligi ukiomba ratiba ya mechi yao ya kwanza ya ligi ibadilishwe.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Saad Kimji, ameeleza kuwa tayari wameshatuma barua kwenye bodi juu ya kusogezwa mbele kwa mechi ya kwanza.
Yanga wameeleza kuwa ratiba ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara inaingiliana hivyo bora wakapata nafasi ya kufanya maandalizi ya CAF kwanza.
Ratiba inaonesha kuwa baada ya kucheza na Township Rollers wikiendi ijayo August 24, Yanga wataanza safari ya kurejea Tanzania na August 28 wataanza kibarua na Ruvu Shooting kunako Ligi Kuu.
Kwa mujibu wa barua, imeeleza kuwa wameomba mechi na Ruvu ipangwe walau kuanzia tarehe 30 kwenda mbele ili wapate nafasi ya maandalizi.




0 Comments