

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Kazi na Ajira, Anthony Mavunde amewataka wananchi hususani wa Wilaya ya Rufiji na Kibiti kuchangamkia fursa zitokanazo na mradi wa uzalishaji umeme wa Stiegler's gorge unaotekelezwa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.
Akizungumza katika kongamano la kujadili fursa , kiuchumi lililoandaliwa na sekta binafsi nchini TPSF, Mhe Mavunde amelitaka Baraza la Uezeshwaji Wananchi Kiuchumi NEEC kushirikiana na Uongozi wa Wilaya ya Rufiji kutoa elimu ya kiuchumi kwa Wanawake na Vijana ili waweze kufanikisha ushiriki wao wa moja kwa moja kwenye mradi huo kupitia ajira zitakazozalishwa na fursa mbalimbali za kiuchumi kwenye mradi huo mkubwa.




0 Comments