Windows

Tutunzeni vyakula vyetu, sitaki nije kuona mnateseka na njaa - Waziri Lugola


Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wananchi kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia.

Waziri Lugola ameyazungumza hayo katika Mkutano wa hadhara wa Wananchi wa Kijiji cha Mwiseni, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola.

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, ameanza ziara jimboni kwake ya kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kupitia kufanya mikutano ya hadhara.


Post a Comment

0 Comments