Na Amiri kilagalila, Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Njombe kuwachukulia hatua watumishi waliosababisha hasara na hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) zisizokuwa za lazima.
Olesendeka ametoa maagizo hayo mkoani Njombe katika kikao cha baraza maalumu la madiwani halmashauri ya mji wa Njombe ili kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali.
“Natarajia ripoti ambayo mkurugenzi utaleta kwa katibu tawala na ofisini kwangu,ili niunganishe na halmashauri nyingine sita pamoja na ofisi yangu kwa pamoja nipeleke ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa lakini ripoti hiyo iwe imeainisha majina ya waliosababisha hoja,vyeo vyao na hatua za nidhamu zilizochukuliwa,”alisema Olesendeka
Aidha halmashauri ya mji wa Njombe imevifikisha mahakamani vikundi 47 vya wajasiriamali ambavyo vimeshindwa kurejesha fedha za mikopo ya asilimia kumi zitokanazo na mapato ya ndani ikiwa na lengo la kuhimiza urejeshwaji ili wahitaji wengine waweze kukopeshwa.
Zaidi ya Mil 98 zimeshindwa kurejeshwa tangu mwaka 2015 hadi sasa jambo ambalo limeibua hoja kwa mkaguzi wa hesababu za serikali CAG ambaye ameshauri halmashauri kuhakikisha zinatoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali na kuzifatilia kwa marejesho ili ziweze kutumika kukopesha wahitaji wengine
Dorcas Mkello Mhazina wa Halmashauri ya Mji wa Njombe akiwasirisha hoja amesema halmashauri imekuwa na changamoto kubwa katika kufatilia wadaiwa wa mikopo ya asilimia kumi na kudai kwamba kitendo hicho kumekwamisha mipango ya halmashauri ya kuwawezesha mitaji wajasiriamali
Hata hivyo licha ya Halmashauri ya Mji wa Njombe kuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa miradi yake lakini ni miongoni mwa halmshauri tano kati ya sita ambazo zimepata hati safi isipokuwa Makete.
0 Comments