Windows

RC Dodoma atoa agizo zito kwa Mkurugenzi Chamwino


Na Enock Magali,Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Dr.  Binilith Mahenge amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya Chamwino kuwasilisha kwake taarifa ya mkakati wa Halamashauri ya Wilaya hiyo juu ya kutaka kulichukua shamba la zabibu la chinangali II lenye jumla ya Ekari 1250 kwa lengo la kulisimamia na kuliendesha shamba hilo.

Hayo yanajiri wakati maendeleo ya shamba hilo kuzorota kwa kukosa huduma muhimu na usimamizi kutoka kwa wananchi waliopewa maeneo ya kulima kwenye shamba hilo.

Aidha, Dr Mahenge ametaka wananchi wote walioshindwa kuhudumia na kusimamia maeneo waliyopewa kwenye shamba hilo na kuyatelekeza, kuandikiwa barua kuwa watanyang'anywa maeneo hayo mara moja.

Akiwa ziarani Wilayani Chamwino, Dr Mahenge ametaka wananchi 120 ambao wao wanahudumia na kusimamia maeneo waliyopewa kwenye shamba hilo wajumuishwe kwenye mkakati huo mpya wa kuliendesha shamba hilo na ametaka Halmashauri ya Chamwino pamoja na kulichukua shamba hilo wahakikishe pia wanaweka mkakati wa kulipa deni la karibu Tsh 2.7 bilioni ambazo zilitolewa na Benki ya CRDB kama Mkopo wa kujenga miundombinu ya maji na umwagiliaji na uendeshaji wa shamba hilo.

Awali mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndg. Athuman Masasi alibainisha kuwa halamshauri imeamua kulichukua shamba hilo na Deni lake lote na kulisimamia kama mradi wa kimkakati ambao kwa tathimini waliyofanya shamba hilo lina uwezo wa kuizalishia Halmashauri yake hadi Tsh 4 Bilioni kwa mwaka kupitia kilimo Cha Zabibu, amesema watawaengua wakulima wote ambao wameshindwa kusimamia maeneo waliyopewa kulima kwenye shamba hilo lenye visima na maji ya kutosha, mabwawa makubwa ya kuhifadhia maji, mashine na miundombinu ya umwagiliaji wa matone.

Post a Comment

0 Comments