Windows

Wafanyabiashara washauriwa kubadilisha fedha za kigeni kwenye Taasisi za Kibenki


Na Timothy Itembe, Mara

Wafanyabiashara wilayani Tarime mkoani Mara wametakiwa kubadilisha Fedha za kigeni katika Taasisiza kibenki ili kuepuka utakatishaji fedha jambo ambalo nikkinyume cha sheria.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja Benki Tawi la Tarime,Joseph Manyanya kwenye kikao cha pamoja na wafanyabiashara kilichoandaluiwa na Benki hiyo ili kujadili msitakabali wa kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuboresha huduma za Benki ya CRDB.

Manyanya alisema kuwa kuna haja wafanyabiashara kufanya miaamala ya kubadilisha fedha za kigeni katika taasisi za kibenki zilizopo kisheria badala ya kufanyamiamala kwenye magenge yasiyosalama kwa hali hiyo itasaidia hasara pamoja na kupunguza utapeli unaoweza kujitokeza.

"Mimi nishauri wafanyabiashara wetu kutumia taasisi za Benki zilizopo kisheria katika swala zima la kubadilisha fedha za kigeni ambapo katika Benki yetu ya CRDB tunatoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kutoka Nchi mbali mbali na tuna mpango ulio jikoni wa kuanzisha huduma ya badilisha fedha za Nchi jirani ya kenya wateje watumie madirisha yetu yaliyopo"alisema Manyanya.

Kwa upande wake, Meneja mahusiano wateja wa mikopo midogo na yakati, Daniel Nyamwivuga alisema kuwa Benki yake imewakutanisha wafanyabiashara pamoja ili kujadili maswala mbali mbali yanayohusiana na maswala ya Kibenki ikiwemo huduma ya kuchukua na kurejesha mikopo.

Nyamwivuga aliongeza kuwa wafanyabiashara waaminifu ndio wanaotakiwa kwenda kuchukua fomu ya kuomba mikopo kwa lengi la kuinua na kukuza kipato ili kupunguza umasikini pamoja na kuongeza Ajira kwa jamii.

Naye Mairo Wansaku mfanyabiashara kwa niaba ya wenzake aliomba taasisi za Benki kupunguza makato ya riba kutoka asilimia 20 hadi ifikia silimia 14 ili kuwawezesha wateja wa Benki kukopa fedha na kurejesha kwa mda mwafaka.



Post a Comment

0 Comments