

Ni maandamano makuu ya kwanza tangu Jumatatu iliyopita ambapo waandamanji waliofunika nyuso zao wengi wao wakiwa vijana walipolivamia bunge na kulitumbukiza eneo hilo ambalo ni kituo cha kiuchumi cha kimataifa katika mzozo zaidi.
Mji wa Hong Kong umeshuhudia mwezi mzima wa maandamano makubwa pamoja na msururu wa makabiliano mengine ya ghasia na polisi yanayotokana na sheria ambayo ingeruhusu washukiwa kupelekwa kushtakiwa China bara.
Musuada huo kwa sasa umeahirishwa kutokana na ghadhabu kutoka kwa raia wa eneo hilo lakini hatua hiyo haijapata ufanisi mkubwa katika kuzima ghadhabu hiyo ambayo imepelekea kubuniwa kwa vuguvugu kubwa linalotaka marekebisho ya kideomkrasia na kusitishwa hali ya kubanwa kwa uhuru wa eneo hilo.




0 Comments