Windows

Sasa Yanga SC kuwavaa Kariobangi Sharks badala ya AS Vita


Yanga SC itamenyana na Kariobangi Sharks ya Kenya Agosti 4, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Hiyo ni baada ya klabu ya AS Vita ya DR Congo kujitoa kwa kubanwa na ratiba ya mechi za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika iliyotoka mwishoni mwa wiki.

Taarifa hii inakuja siku moja baada ya Yanga SC kushinda mechi ya tatu mfululizo jana katika kambi yake ya Morogoro kujiandaa na msimu upya baada ya kuichapa ATN 7-0 Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro.



Post a Comment

0 Comments