

Watu wasiopungua 70 wameuawa na wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Waokoaji wamegundua miili iliyotapakaa kila pahali katika kijiji cha Ngazai kufuatia shambulizi hilo la wikendi. Idadi kubwa ya miili ilipatikana misituni ikiwa na majeraha ya risasi.
Awali siku ya Jumapili, gavana wa Borno aliambia Xinhua kwamba watu 55 waliuawa kwenye shambulizi hilo la siku ya Jumamosi.



0 Comments