Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya lori la mafuta kuanguka na kusababisha mlipuko mkubwa katika kijiji kimoja katika mkoa wa Benue nchini Nigeria,kulingana na taaridfa zilizotolewa na viongozi wa mitaa na mashahidi hivi jana.
Takriban miili kumi imeweza kupatikana, huku wengine wasiopungua 50 wamethibitishwa kujeruhiwa kutokana na mkasa huo uliotokea katika kijiji cha Ahumbe siku ya Jumatatu, polisi wa usalama wa barabara walisema.
Hata hivyo, mashahidi walisema kuwa takriban watu 50 waliaga dunia baada ya kuchomwa na moto huo uliokuwa ukienea kwa haraka katika barabara kuu ya Makurdi-Aliade.
Wengi wa waathirika walikuwa watu ambao walijaribu kuchota mafuta kutoka kwenye lori hiyo,alisema Aliu Baba, mkuu wa usalama wa barabara huko Benue.
0 Comments