Windows

Jibu la Lulu Diva kuhusu penzi lake la Jaguar


Mkali anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva,‘Lulu Diva’, amesema hatoki kimapenzi na staa wa muziki kukoka Kenya, ‘Jaguar’ bali ni marafiki na wanatarajia kutoa wimbo wa pamoja.

Lulu Diva, amelazimika kuyasema hayo mara baada ya picha zao kusambaa mtandaoni na kuibua tetesi za kuvishwa pete ya uchumba na msanii huyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Starehe jijini Nairobi.

Akizungumza Diva alisema: “Jaguar ni mshikaji wangu, anapenda kazi yangu na mimi ni shabiki yake, tunatarajia kuachia ngoma moja ambayo tumeshaanza kuifanya pia picha ambazo zinasambaa mtandaoni nilikwenda Kenya kumtembelea na siyo Dubai”

Post a Comment

0 Comments