Chama cha TLP kimemteua Rais Dk. John Magufuli kuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amesema Halmashauri Kuu ya TLP ilifanya uteuzi huo ilipokutana miezi miwili iliyopita.
Akizungumzia uteuzi huo amesema Rais huyu ni bora, tukimpoteza, hatupata mwingine. Hivyo ameeleza kuwa wanachama wa TLP na viongozi wake waishangaa CCM, kwani hawaoneshi kutambua mchango na utumishi uliotukuka wa Rais Dk Magufuli.
Ameweka wazi kuwa chama hicho kitamuunga mkono kwenye uchaguzi ujao.
0 Comments