Msanii anayekuja vizuri kwenye Bongo Fleva, Careen Gardner ‘Malkia Careen’ amefunguka kuwa roho yake itatulia kama atafanya kazi na mwanamuziki mahiri Bongo, Christian Bella. Careenaliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa kila mwanamuziki anakuwa na ndoto za kufanya kazi na mwanamuziki mmoja ampendaye hivyo kwa upande wake anatamani kufanya na Bella.
“Kwa kweli moyo wangu utafurahi sana siku nitamtia mikononi Bella ndiyo ndoto yangu ya siku zote itakapotimia. Hata alipofanya na Hamisa Mobeto kwa kweli nilipenda mno ila naamini ipo siku ndoto yangu itatimia,” alisema Careen.
The post CAREEN ATASUUZIKA AKIMNASA CHRISTIAN BELLA appeared first on Global Publishers.
0 Comments