Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe amesema matukio ya utekaji ni Utamaduni mpya unaendelea nchini ambao utaiondolea nchi sifa, huku akieleza kusikitishwa na kitendo cha Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge.

Akizungumza na waandishi wa nje ya Mahakama Kuu, Membe amesema "Huu ni utamaduni mpya ambao haukubaliki na ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba suala la utekaji na watu kupotea linaweza kuiondolea nchi yetu heshima duniani tangu tupate uhuru, hivyo ningependa kuwaomba viongozi wote walikemee," amehoji Membe.

"Jambo la Tundu Lissu kuvuliwa ubunge kama Mtanzania na mimi nilishangazwa, sasa tusubiri Lissu aje nina uhakika kabisa atakwenda Mahakamani, kama kuna haki ataipata Mahamakani" ameeeleza.