Mbali na kutangaza tenda ya kusaka wakala wa kuuza jezi na bidhaa zake, Yanga imetangaza kusaka Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mshindano ikitangaza nafasi hizo kupitia gazetini
Nafasi nyingine zilizotangazwa ni Mkurugenzi wa benchi la Ufundi, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, MKurugenzi wa Masoko, Mauzo na Matukio na Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama
Nafasi ya Katibu Mkuu imekuwa ikikaimiwa na Omary Kaya aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya kujiuzulu kwa Charles Mkwasa kutokana na matatizo ya kiafya
Sifa anazopaswa kuwa nazo mgombea wa nafasi hizo ni Shahada pamoja na uzoefu usiopungua miaka saba katika sekta ya michezo wa soka Kitaifa na Kimataifa
Uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla umedhamiria kuiendesha timu hiyo kisasa kwa kuajili wataalam tofauti na zamani ambapo nafasi hizo zilikuwa zikikaliwa na watu wasiokuwa na sifa au utaalam husika
0 Comments