Windows

Kindoki alikuwa na matatizo ya kutetemeka - Pondamali



Kocha wa makipa wa klabu ya Yanga Juma Pondamali amesema mlinda lango Klaus Kindoki alikuwa na matatizo mengi ya kiufundi likiwemo la kutokujiamini awapo langoni

Aidha, Pondamali anayewanoa makipa wa Yanga tangu mwaka 2015, amesema mlinda lango huyo alikuwa na imani potofu kuwa amerogwa

Pondamali amesema alifanya kazi ya ziada kumuimarisha Kindoki na matunda yake yalionekana wakati ligi inaelekea ukingoni akawa kipa namba moja

"Nilimfundisha jinsi ya kusimama na kudaka mipira bila ya kutema," alisema Pondamali aliyewahi kutamba akiwa mchezaji Yanga na timu ya Taifa

Hata hivyo Pondamali amethibitisha kuwa Kindoki hataitumikia Yanga msimu ujao

"Licha ya kiwango chake kuimarika, kocha alisema kipa wa kigeni anapaswa kuwa namba moja hivyo baada ya kumsajili kipa kutoka Bandari Fc, Kindoki hatutakuwa nae msimu ujao"

Kindoki bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga hivyo huenda akatolewa kwa mkopo au mkataba wake ukavunjwa

Post a Comment

0 Comments