Windows

Usajili utatubeba ligi ya mabingwa - Mwakalebela



Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema usajili wa timu hiyo ulilenga kuunda kikosi imara kwa ajili ya michuano yote msimu ujao

Hivyo nafasi waliyoipata ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao, imekwenda sawa na malengo yao kutokana na aina ya wachezaji ambao wamewasajili

Baada ya Yanga kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa, kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa wadau ambapo wapo wanaodhani aina ya usajili uliofanywa na Yanga mpaka sasa hautaisaidia timu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa

Mwakalebela amesema lengo lao kuu lilikuwa kufanya vyema katika mashindano yote ambayo watashiriki msimu ujao ndio maana wamesajili wachezaji wenye vipaji na uwezo mkubwa

"Kiukweli ilikuwa mipango yetu kukiimarisha kikosi chetu kwa kusajili wachezaji wa kiwango cha juu na wenye kuweza kutoa ushindani, kama mnavyoshuhudia, tunajua kufanya hivi ni kutekeleza matakwa ya mwalimu, hapo jukumu litabakia kwake," amesema Mwakalebela

"Tumepokea kwa furaha taarifa ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao"

"Viongozi tumefurahi, Zahera pia amefurahi, kilichobaki ni kujipanga ili kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michuano hiyo"cut

Yanga na KMC zimepata nafasi kuungana na Simba na Azam Fc ambazo zilijihakikishia nafasi mbili za awali kabla ya CAF kuthibitisha kuongezwa kwa idadi ya timu kutoka mbili na kuwa nne

Kushiriki michuano ya Kagame

Yanga pia imealikwa kushiriki michuano ya kombe la Kagame inayofanyika Rwanda kuanzia Julai 07 hadi Julai 21 2019

Mabingwa hao wa kihistoria watakuwa na nafasi ya kujaribu 'silaha' zao mpya kwenye michuano hiyo

Aidha michuano ya Kagame inayoshirikisha vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, itakuwa fursa kwa Yanga, Simba na Azam Fc kujiandaa na mashindano ya CAF ambayo hatua ya awali inaanza mwanzoni mwa mwezi wa nane

Post a Comment

0 Comments