Licha ya Zimbabwe kutolewa kwenye mashindano ya COSAFA hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati na Zambia, kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji walion'gara kwenye michuano hiyo
Kamusoko alicheza mechi zote mbili za robo fainali na nusu fainali huku akiibuka nyota wa mchezo wa robo fainali dhidi ya Comoros
Katika michuano hiyo Kamusoko alikuwa injini ya Zimbabwe sehemu ya kiungo cha chini, akikaba na kuanzisha mashambulizi na wakati mwingine kwenda kushambulia mwenyewe
Hakuna shaka Kamusoko atakuwa sehemu ya kikosi cha Zimbabwe ambacho kitashiriki michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Misri baadae mwezi huu
Hii ni nafasi nzuri kwa viongozi wa Yanga kutathmini kama wanapaswa kumuacha kiungo huyo au kumuongeza mkataba
Hakuna shaka Kamusoko kiwango chake kimeimarika sana na pengine bado anahitajika sana katika kikosi cha Yanga
0 Comments