HIVI karibuni jarida la Forbes lilimtaja msanii Jay Z (Shawn Corey Carter) kuwa msanii mwenye utajiri mkubwa zaidi duniani. Akiwa na utajiri wa Dollar za Marekani Zaidi ya Bilioni Moja kutokana na muzik na kuwekeza katika kampuni ya Tidal ambayo inauza muziki mtandaon.
Wasanii wengine waliotajwa kwenye Top 5 ya wasanii wenye utajiri mkubwa zaidi duniani ni Dr. Dre, ambaye anashika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa Dola za Marekani zaidi ya milioni 800. Msanii anayeshika nafasi ya tatu ni Sean John Combs ( Diddy) ambaye ana utajiri usiopungua Dola milioni 740.
Wasanii wengine waliotajwa na jarida hilo ni Kanye West, ambaye anashika nafasi ya nne huku akiwa na utajiri usiopungua Dola mil. Marekani 240. Msanii Drake ndiye anayyefunga orodha hiyo ya Top 5 akiwa na utajiri wa Dola zisizopungua milioni 150. Utajiri wa wasanii hawa unatokana na kazi zao za muziki na biashara mbalimbali wanazofanya.
The post Wasanii wa Hip Hop Matajiri Zaidi Duniani appeared first on Global Publishers.
0 Comments