

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema michakato ya usajili katika klabu hiyo ndio imeanza rasmi jana na wataendelea kutoa taarifa kwa kila usajili uliokamilika
Jana Simba ilitangaza kumuongezea mkataba nahodha wake John Bocco ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kubaki na mabingwa hao wa Tanzania Bara
"Tunawataka wanachama na mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi, tumeanza rasmi kusajili na taarifa zote zitakazokuwa zimekamilika zitakuwa zikitolewa kwao," amesema
"Tumejipanga kusajili wachezaji tunaowahitaji kwa gharama yoyote, kikubwa tuwe na tubira," amesema
Inaelezwa Simba huenda ikasajili wachezaji saba wa kigeni ikiachana na idadi hiyo ya wachezaji
Juuko Murshid na Emmanuel Okwi tayari wamejiengua wenyewe wakati Nicholas Gyan, Zana Coulibaly na Asante Kwasi nao wako hatarini
Aidha bado mwafaka haujafikiwa kuhusu viungo Haruna Niyonzima na James Kotei kwani licha ya kupendekezwa waachwe na kocha Patrick Aussems, sehemu kubwa ya mabosi wa Simba wanaona wachezaji hao bado wana nafasi ya kuendelea kuichezea Simba
Lengo la Simba ni kuongeza wachezaji wengi wenye hadhi ya Kimataifa zaidi ili kuisaidia timu hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao



0 Comments