

Alhamisi ya Juni 13 2019 wenyeji wa michuano ya AFCON 2019 MIsri wataumana na Tanzania katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa uwanja wa Borg Al Arab katika jiji la Alexandria
Chama cha soka cha Misri kimechapisha tiketi 30,000 ambazo zimeanza kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri
Misri imeuchukulia mchezo huu kwa uzito mkubwa kwani utakuwa mchezo wao wa kwanza wa kirafiki kujipima baada ya maandalizi ya muda mrefu kuelekea michuano hiyo
Winga wa Liverpool Mohammed Salah anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Misri kwenye mchezo huo
Aidha kwa upande wa Tanzania hiki ni kipimo sahihi kwa kikosi cha Emmanuel Amunike ambacho kimepangwa kundi C na vigogo wa soka Barani Afrika Senegal na Algeria pamoja na wapinzani wao kutoka Afrika Mashariki, Kenya
Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki nchini Misri kwani baada ya mchezo wa keshokutwa, itashuka tena dimbani baada ya siku chache kuumana na Zimbabwe kabla ya michuano kuanza
Baada ya michezo hiyo Amunike anatarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachoshiriki michuano hiyo



0 Comments