Windows

Shikalo anasubiri muda muafaka atue Yanga



Uongozi wa Yanga umetangaza kusitisha michakato ya usajili wa wachezaji wa Kimataifa baada ya kukamilisha usajili huo kwa asilimia 95

Juzi Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema Yanga tayari imewasajili wachezaji wote wa kigeni waliopendekezwa na kocha Mwinyi Zahera hivyo kwa upande wao wamemaliza kazi

Lakini wengi wamekuwa wakijiuliza juu ya hatma ya mlinda lango wa Bandari Fc, Mkenya Farouq Shikalo ambaye jina lake sio miongoni mwa yaliyotangazwa kutua Yanga kwenye Harambee ya Kubwa Kuliko iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee mwishoni mwa wiki

Hata hivyo inaelezwa Shikalo ni miongoni mwa wachezaji ambao wataitumikia Yanga msimu ujao, hakuwekwa hadharani kwa kuwa mchakato wake wa usajili haukuwa umekamilika

Juzi baada ya mchezo wa kirafiki kati ya DR Congo dhidi ya Kenya uliofanyika nchini Hispania, Zahera alipata nafasi ya kuonana na mlinda lango huyo ambapo inaelezwa waliweka sawa mchakato wa ujio wake Jangwani

Ujio wa Shikalo unakamilisha idadi ya nyota tisa waliosaini mikataba, Kindoki akiwa wa 10

Hata hivyo nafasi ya Kindoki huenda akasajiliwa mchezaji mweingine kwani upo uwezekano mkubwa mkataba wake utasitishwa

Post a Comment

0 Comments