Windows

Rais CAF akamatwa kwa tuhuma za rushwa



Rais wa Shirikisho la soka Barani Afrika, Ahmad Ahmad anashikiliwa na Polisi nchini Ufaransa kwa tuhuma za rushwa

Kwa mujibu wa mtandao wa Jeune Afrique, Rais huyo amekamatwa na Polisi wa kuzuia rushwa nchini Ufaransa majira ya saa mbili na nusu leo akiwa kwenye Hoteli aliyofikia Mjini Paris.

Ni Hotel ambayo alikuwa akikaa wakati akihudhuria mkutano Mkuu wa FIFA.

Kwa mujibu wa vyanzo vya mtandao huo ni kwamba kukamatwa kwa Ahmad Ahmad huenda kumetokana na tuhuma ya matumizi mabaya ya ofisi ambayo yalifichuliwa na aliyekuwa katibu Mkuu wa CAF Amr Fahmy

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limeeleza kufuatilia tukio hilo na limetaka kupatiwa taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka nchini Ufaransa

Post a Comment

0 Comments