Windows

Rafu Mbaya! Mfungaji Aliyeletwa na Simba Asaini Yanga – Video

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda na Klabu ya Police FC ya Uganda, Juma Balinya, mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa miaka miwili.

Balinya ambaye ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Uganda 2018/19 inayodhaminiwa na StarTimes, ametambulishwa na uongozi wa Yanga mbele ya wanachama wa klabu hiyo katika hafla ya kuichangia Yanga inayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kwamba Balinya ambaye ana mabao 19, alitua nchini hapo jana akiwa ameletwa na Klabu ya Simba lakini Yanga  SC wamefanya yao kwa kumuiba na kumsainisha mkataba huo.

Mbali na Balinya, Yanga imemtambulisha mchezaji mwingine, Abdul Aziz Makame,  anayetokea timu ya Mafunzo ya Zanzibar, ambaye wanamwita ‘Pacha wa Fei Toto’

 

The post Rafu Mbaya! Mfungaji Aliyeletwa na Simba Asaini Yanga – Video appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments