Windows

KAZI IPO… ‘WIKI YA MWANANCHI’ KUITIKISA TANZANIA

MWENYEKITI wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga,  Anthony Mavunde,  amesema wamependekeza kwa uongozi kuanzisha wiki maalum itakayoitwa ‘Wiki ya Mwananchi’, itakakayokuwa maalum kwa ajili ya wapenzi na wanachama wa Yanga kuitumikia jamii.

 

Amesema wiki hiyo itakuwa ikifanyika mwezi Agosti kila mwaka na siku ya kilele chake kutafanyika tukio kubwa litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam likiambatana na utambulisho wa wachezaji wao wapya.

“Tumepanga tuwe na Wiki ya Mwananchi’, ambapo wanachama wa Yanga watafanya usafi maeneo katika hospitali, masoko na kutoa misaada mbalimbali. Wiki hiyo ikikamilika tutakutana Uwanja wa Taifa”.

 

Amesema wamemuomba Rais Magufuli na endapo ataridhia tukio hilo litafanyika mwaka huu ambapo miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni kutambulisha wachezaji wao wapya wanane ambao wamesajiliwa kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya msimu ujao.

The post KAZI IPO… ‘WIKI YA MWANANCHI’ KUITIKISA TANZANIA appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments